Kikundi cha Jakaya Group kutoka Lizaboni waibuka washindi wa kwanza kwa mara ya pili katika mashindano ya Ngoma za Asili kwenye Tamasha la Majimaji Selenbuka 2016 lililofanyika kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, Ruvuma kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 04 Juni 2016.

Tamasha la majimaji selebuka ni tamasha linalofanyika kila mwaka mjini Songea tangu lilipoanzishwa mwaka 2015.

Tamasha linahusisha vitu vifuatavyo;

  1. Riadha (Marathon)
  2. Ngoma za Asili (Traditional Dances)
  3. Mdahalo kwa shule za Sekondari (Schools Debate)
  4. Utalii wa ndani (Local Tourism)
  5. Mbio za Baiskeli (Cycling)
  6. Maonyesho ya Ujasiliamali na biashara (Trade Fair and Entreprenuership).

Tamasha litafanyika tena kuanzia Tarehe 23 hadi 30 Julai 2017.