Tourism

thumb_DSC_5529_1024

cropped-thumb_dsc_5529_1024.jpg
Mbababay Beach Nyasa
thumb_DSC_7016_1024
Matogoro Forest and Mountains

thumb_DSC_5519_1024

imageedit_16_6124042443

IMG_0188IMG_0199IMG_0253img-20160602-wa0035

img_0236
Luhira Maliasili
img_0247
Luhira Maliasili
img_0229
Luhira Uvuvi

img_0188

img-20160602-wa0035
Matogoro Forest Reserve in Songea Ruvuma Tanzania.

Mbali na burudani ya ngoma za asili zilizokonga nyoyo za wananchi waliohudhuria tamasha hilo, pia kulikuwa na utalii katika vivutio mbalimbali vilivyoko mkoani humo kama vile hifadhi ya mbuga za wanyama ya Luhira, hifadhi ya misitu ya Matogoro (Matogoro Forest Reserve), mradi wa ufugaji wa samaki katika mabwaba ya Ruhila, sehemu zote zipo kilomita chache kutoka Songea Mjini.
Siyo hayo tu, pia washiriki walipata nafasi ya kujionea mfano wa kuigwa kwa wanamke kutokana na mradi mkubwa wa ufuaji umeme eneo la Tulila, lililopo zaidi ya kilomita 50 kutoka Songea Mjini. Huu ni mradi ulioanzishwa na huendeshwa na masista tu wa Kanisa la Mtatifu Benedict. Chochote kile katika mradi huu huendeshwa na wao na katu huwezi kukutana na sura ya kiume hata awe mlinzi!  Wao ndio hukesha wakibadilishana zamu ya kukontroo mitambo, ukarabati wa aina yoyote ile hufanywa na wao tu!
Kwa kweli ilikuwa ni zaidi ya maajabu, hasa kuzingatia ukubwa wa mradi ambao umeme wake ndiyo kutoia huduma mjini Songea nzima pamoja na wilaya jirani. Ni mradi mkubwa sana ambao huwaingizia mamilioni ya fedha kila mwezi kwa huduma yake.
Mbali na mradi wa umeme, pia upande wa pili masista wa kanisha hilohilo lakini wao wakitokea Chipole, waliwashangaza wengi kwa ubunifu wa bidhaa mbalimbali, ambazo kwenye maonyesho ya ujasiriamali zilishika nafasi ya pili. Miongoni mwa bidhaa zao zilizokubalika zaidi ni mvinyo uliyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na mishumaa na soseji.
Siyo hayo tu, washiriki pia walitembelea mradi wa ufugaji samaki katika Mabwawa ya Ruhila na kupata kupewa elimu juu ya ufugaji.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: