Schools Debate

imageedit_20_5192710038

Mdahalo ‘debate’ kwa shule za sekondari

washindi-wa-kwanza-mpaka-wa-tatu-kwenye-mdahalo-2016

SO-MI na Tanzania Mwandi katika kuthamini msingi wa maendeleo mashuleni mkoani Ruvuma, Tamasha la Majimaji tangu kuanzishwa kwake wamekuwa wakiratibu mihadalo kwa shule za sekondari ambapo mwaka huu mwitikio ulikuwa mkubwa zaidi.
Tofauti na mwaka jana ambapo shule tano ndizo zilizoshiriki, mwaka huu zilishiriki jumla ya shule 11, huku pia waratibu wakiboresha zaidi zawadi kwa washindi, kwa kutoa IPad kwa shule tatu zilizofanya vizuri, IPad zenye notice ya masomo yote kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita kama sehemu ya kuwarahishia ufaulu kwenye mitihani yao. Shukrani za kipekee ni kwa Shirika la Maendeleo la Kijapani (JICA) waliotoa sapoti hiyo ya IPads.
Shule ya De Paul iliibuka kidedea ikifuatiwa na St. Agness huku Shule ya Wasichana ya Songea ikishika nafasi ya tatu, ambapo mbali na IPad washindi wote walitunukiwa ngao ya ushindi. Shule ya Kingosera ambayo ilikuwa ikitetea ubingwa wake wa mwanzo, iliambulia patupu safari hii, huku ikikosekeana hata kwenye Tatu Bora licha ya kuanzia hatua ya mtoano moja kwa moja.
Mkurugenzi Mwakilishi wa JICA, Toshio Nagase aliambatana na wajumbe wenzake wa shirika hilo, Jacob Katanga, Kei Umetsu, Zuhura Mwakijinja, walihudhuria mdahalo huo wakiungana na mwanachama wa JATA, wakili Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni Mkurugenzi Mwenza wa Asasi ya SO-MI.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: