MREJESHO WA TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA KUTOKA KWA BALOZI WA TAMASHA BWANA NATHAN MPANGALA LILILOFANYIKA MWISHONI MWA MWEZI WA TANO MJINI SONGEA, MKOANI RUVUMA 2016.
Balozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka, Nathan Mpangala ambaye pia ni mchora vibonzo akitoa mrejesho kuhusu tamasha la Majimaji Selebuka katika mkutano wa wadau uliofanyika mwishoni mwa wiki uliofanyika katika ukumbi wa ‘Nafasi Art Space’ uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Tamasha la Majimaji Selebuka lilifanyika Songea, mkoani Ruvuma mwishoni wa mwezi wa tano mwaka huu.
Baadhi ya wadau waliojitokeza kwenye mkutano wa mrejesho kuhusiana na tamasha la Selebuka wakifuatilia makala ya video iliyokuwa ikionesha matukio mbalimbali kuhusiana na tamasha hilo.
Balozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka, Nathan Mpangala (aliyenyoosha mkono) akifafanua jambo kwa wadau hao. Balozi huyo amewashukuru watu wote waliojitokeza na kuchangia maoni.
Washindi watano kwa upande wa watoto wakiwa na Zawadi zao pamoja na vyeti walivyopewa kupitia Majimaji Selebuka Mtu kwao Forum kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2016.

