Bingwa wa Riadha kwa upande wa wanawake 21Km, Neema Mswadi akichanja mbuga.Kinara wa mbio za 42km kwa wanawake, Fabiola William kwenye Marathon iliyoandaliwa na Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea mjini Songea, Ruvuma.Bingwa wa 42km kwa wanawake, Fabiola William kulia akiwa na mshindi wa pili, Neema Kisuda wakihakikisha kama kweli mkwanja waliopewa umetimia.Bingwa wa mbio za walemavu 21km, Bwana Shukuru Halfan akichanja mbugaMmoja wa washiriki wa Paralympic akinyweshwa maji baada ya kumaliza mbio za 21Km katika viwanja vya Majimaji mjini Songea.Baadhi ya washiriki wakishuhudia zoezi la utoaji zawadi kwa washindiBingwa wa 42km kwa wanawake, Fabiola William akikabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Ruvuma, Christian Matembo.
2.TRADITIONAL DANCES
Kikundi cha Ngoma cha Ruvuma Championi, kikifanya yake jukwaani kwenye fainali ya ngoma za asili katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Ruvuma.Ruvuma champion pamoja na waandaaji wa tamasha la Majimaji Selebuka
Kikundi cha Ngoma ya Mganda kutoka Luhagala wakionyesha manjonjo katika kusaka mkwanja wa ubingwa
Washindi wa mashindano ya Ngoma za Asili kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea kufanyika mjini Songea katika viwanja vya Majimaji.